Ads (728x90)

Powered by Blogger.


 Na Albano Midelo
Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Augustino Mjimwema Songea Dayosisi ya Ruvuma wamechanga zaidi ya shilingi milioni 57 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa.


Katibu wa Kanisa hilo Dk.Daniel Mtamakaya amesema ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo zinahitajika zaidi ya shilingi milioni 186 ambapo hadi sasa fedha zinazohitajika ni zaidi ya milioni 129.
 
Katibu Mkuu huyo alisema Kanisa limefanikiwa kuchangisha zaidi ya shilingi milioni 33 ambazo zitatumika kwa ajili ya kuezeka Kanisa hilo na kwamba kinachohitajika hivi sasa ni shilingi milioni 15 za gharama za fundi.
 
Kwa mujibu wa Katibu huyo Kanisa hilo pia limejenga shule ya Jumapili (Sunday School) ambayo ujenzi wake utagharimu zaidi ya milioni tano hadi utakapokamilika katika miundombinu yake.
“Mara tu baada ya kuezeka Kanisa jipya, Kanisa dogo linalotumika sasa, litabadilishwa matumizi ili liwe nyumba ya kuishi wahudumu ili kuepuka kulipa pango ambayo hugharimu alisema Dk.Mtamakaya.
 
Akizungumza baada ya kupata taarifa ya ujenzi wa kanisa hilo, Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Ruvuma Mhashamu Raphael Haule amewapongeza waumini wa Kanisa hilo  wapatao 775 kwa kugharamia ujenzi huo na kuanzisha shule ya watoto.
 
Hata hivyo amesema Kanisa linaendelea kufanya jitihada za kutafuta wafadhili wa ndani na nje ya nchi ili kuharakisha ujenzi wa Kanisa hilo ambalo kwa asilimia kubwa zimetumika nguvu za waumini wenyewe. “Najaribu kuwasiliana na wafadhili wa ndani na nje ya nchi, baadhi ya wafadhili toka nchini Ujerumani wamefika hapa kuangalia Kanisa hili,naamini Mungu atatupa fedha za kuezeka na kukamilisha ujenzi wa Kanisa hili’’, alisema Mhashamu Haule. Anatoa wito kwa watu wote wenye mapenzi mema kutoka ndani na nje ya nchi kutoa mchango wowote ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo ambalo kwa kiasi kikubwa Waamini wamejitoa kikamilifu.


Post a Comment