Na Titus
Amigu
Ndugu yangu, mwanzoni mada hii inaweza kuonekana ngumu kidogo lakini ukiisoma kwa uvumilivu utagundua kwamba siyo ngumu. Basi, isome kwa uvumilivu kidogo. Ni hivi, katika suala la kunywa mvinyo (pombe au divai), watu tunatuingia katika ubishi wa kijinga. Ni kwamba tunapobisha tunajionesha wenyewe kwamba tumeachwa nyuma kabisa katika uelewa wa mambo kisayansi, hapa kwa namna ya pekee, Kemia. Maana yake sisi ni mbumbumbu wa Kemia. Pole kwa lugha hii kali, lakini ndiyo inayoelezea mada yangu vizuri.
Peke yangu sishangai sana mkasa huu. Waafrika tunayakimbia sana masomo ya sayansi na mara nyingi kwa sababu ya kutushinda nasi kuyachukia huwa tunayabatiza majina ya kila namna. Hivi karibuni, huko shuleni au vyuoni, masomo kama Hesabu, Biolojia, Fizikia na Kemia yamekuwa yakijulikana kwa jina la utani la “Baba Mkwe”.
Lakini, moja ya matokeo ya kukimbia kwetu masomo ya sayansi ndiyo ubishi huu juu ya kilevi (alcohol) ninaotaka kuwalengesheeni nyie wote. Katika makala hii “alcohol” itamaanisha kilevi kilicho kiini cha pombe (divai au mvinyo). Ubishi huu ni ishara dhahiri ya ujinga wetu. Yaani hatujui pombe ni nini. Ndipo wataalamu wanatucheka na kutuona wote kuwa wajinga. Ajabu, Wakristo wanaobisha siyo tu wasiosoma bali hata wanaodhaniwa ni wasomi. Kwa vyovyote, kwa kusoma kwao, mambo mengine wanayobisha yalipaswa yamalizike kwa elimu ya shule ya msingi au sekondari tu, lakini wapi!
Mfano wa suala la pombe unatosha sana. Ni hivi, kwa sababu ya ujinga, wapo Wakristo wanaodai hawataki kabisa kuiona pombe sembuse kuigusa na kuitumia. Narudia, ubishi huu unaotokea kwenye ujinga tu katika sayansi.
Sikilizeni. Katika maisha ya sasa, hakuna mwanadamu hata mmoja anayeweza kuikwepa kabisa “alcohol”. Hakuna ufundi wowote wa kuikwepa pombe. Kwa nini? Kwa sababu tunagusana nayo kila siku na tunakula au tunainywa kila siku. Nisikilize. Ni hivi, kisayansi, pombe inapatikana kwa uchachushaji sukari.
Mambo
huendaje? Nisikilize tena. Mara nyingi sana mchakato wa uchachushaji katika
vyakula hufanywa na vijimelea vidogo ambavyo huingia kwenye vyakula na
hufanyika pasipo sisi kujua. Kumbe, sisi tunaojidai wajanja wakati tu wajinga,
tunapumbazika tu kwa kutoelewa sawasawa haya.
Katika elimu ya Kemia, “alcohol” inapatikana katika kubadilika molekyuli za sukari kwenda kuwa “alcohol” na hewaukaa (yaani carbon dioxide) kwa kutumia fomula hii: C6H12O6 → 2CO2 + 2C2H5OH.
Katika elimu ya Kemia, “alcohol” inapatikana katika kubadilika molekyuli za sukari kwenda kuwa “alcohol” na hewaukaa (yaani carbon dioxide) kwa kutumia fomula hii: C6H12O6 → 2CO2 + 2C2H5OH.
Katika elimu ya Kemia “alcohol” ni kemikali itokanayo na mimea(organic compounds). Kwa hali hii, kemikali hii hutengenezwa kwa viasili (elements)vilivyomo kwenye mimea. Katika mabara mengine, zabibu ni maarufu sana katika kutengeneza “alcohol”. Lakini hapa kwetu Afrika, njia kuu ambayo “alcohol” (ethyl alcohol) hupatikana ni kwa wanga uliomo kwenye mimea kama vile mahindi, mtama, uwele, ngano, shayiri nk., kubadilishwa kuwa sukari na hatimaye sukari kuwa “alcohol” kwa njia ya bakteria au hamira.Ndiyo maana tuna pombe kama “bia”, “myakaya”, “kangara”, “komoni”, “chibuku” na kadhalika.
Tusidanganyike. Ikiwa “alcohol” huhitajika kwa kiwango kikubwa, viwanda maalumu hutumika, mfano viwanda vya TBL; na ikiwa huhitajika kwa kiasi kidogo tu hutengenezwa kwa njia za kienyeji majumbani na vijijini mwetu.
Lakini si hivyo tu. Wakati mwingine “alcohol” huweza kupatikana kutokana na vyakula vya aina ya wanga tuviandaavyo kila siku au sukari tuitumiayo kila siku majumbani mwetu kwa njia iitwayo“uchachushaji”(fermentation).
Tunapofumbika
macho wengi ni ukweli kwamba, mara nyingi mchakato wa uchachushaji katika
vyakula hufanywa na vijimelea vidogo sana ambavyo huingia kwenye vyakula na
hufanyika pasipo sisi kujua kwa sababu macho yetu ya nyama hayana uwezo wa
kuviona. Kwa kisa hicho, kiasi cha “alcohol” ambacho hutokea pia huwa kidogo
sana kuweza kung’amua uwapo wake.
Ndipo basi, hata utengenezaji wa mikate huhusisha uzalishaji wa “alcohol” kwa sababu hamira huhusika katika uchachushaji ili mkate upande.Unga wa ngano usipopanda hauwi mkate bali donge la unga (“bumunda”) tu. Hapa hapa tuhabarike, siku hizi kuna akina mama ntilie wakorofi kadhaa wanaopandisha unga wa mahindi kwa hamira ili ugali upatikane mwingi kwa unga kidogo.
Hata hivyo, kiasi cha “alcohol” kipatikanacho
huwa ni kidogo sana kuweza kuutambua uwepo wake. Kumbe, “alcohol” ipo nasi
kushoto na kulia, juu na chini. Kifupi, ninachotaka kusisitiza ni kwamba
hatuwezi kukwepa kutumia “alcohol” katika maisha yetu ya kawaida ya kila siku.
Hatuna ujanja huo.
Narudia. Ni kwa sababu mara nyingi tunakumbana na “alcohol” kwenye vyakula vyetu tulavyo pasipo sisi wenyewe kujua. Tunakumbana na “alcohol” kwenye mikate,kwenye sukari, na kwenye vyakula vya wanga pasipo sisi kujua. Tunakumbana na “alcohol” kwenye vinywaji mbalimbali baridi na matunda pasipo sisi kujua kwa sababu kiasi cha “alcohol” (alcohol concentration) kilichomo humo huwa ni kidogo sana kuweza sisi kung’amua uwapo wake.
Kwa hali halisi, katika michakato kama hiyo wanadamu wote tunakutanishwa pia na “alcohol” ingawaje kwa kutojua kwetu tunadhani hatujakutana na “alcohol” yoyote. Labda tu wajinga tunaoishi kwa kanuni ya “kwa kuwa sioni kitu maana yake hakipo”. Kipimo chetu ni macho tu, kisichoonekana kwa macho eti hakipo. Kumbe, ndivyo tunavyodanganyika mbele ya bakteria, virusi na vimelea vinginevyo. Basi, hapa tuhabarike vyema.
Kumbe, kwa ukweli huu, hata mkate nao una kiasi cha “alcohol”. Je, ni wangapi wasiokula mikate katika dunia ya leo? Kama umekula na bado unakula maana yake umeshakula pombe tayari. Je, utaitema leo au hutaigusa tena?
Ndugu yangu, mkate una pombe ndani yake. Kwa vipi? Kisayansi, hakuna unachokwepa. Ni hivi, katika utengenezaji wa mikate huhusika pia “alcohol”(kilevi) kwa sababu hamira (yeast) huhusika na hatua hii ya uchachushaji kusudi mkate upande. Kwa bahati mbaya au njema, kiasi cha “alcohol” kipatikanacho kwenye mkate huwa ni kidogo sana kuweza kuutambua uwepo wake lakini maana yake ipo. Unanielewa? Kama unakubali katika mkate KUNA KIASI KIDOGO CHA POMBE, MAANA YAKE IPO.
Usinikodelee
macho maana yake ndiyo hii, muulize mtu yeyote anayejua lugha atakubaliana na
mimi. Ni kama ningekuambia ndani ya kahawa kuna caffeine au cocaine kwa kiasi
kidogo. Hii inamaanisha vile vile kwamba ipo.
Lakini kwa watakao kukwepa pombe, kiasi gani ndiyo haramu? “alcohol” nyingi au kiasi chochote? “Alcohol” ipi ni haramu, inayoonekana tu au na isiyoonekana pia? Kwa hali hii ya mambo, kumbe, ukweli wenyewe ni kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kuepuka kugusa au kutumia “alcohol” katika maisha yake ya kila siku.
Lakini kwa watakao kukwepa pombe, kiasi gani ndiyo haramu? “alcohol” nyingi au kiasi chochote? “Alcohol” ipi ni haramu, inayoonekana tu au na isiyoonekana pia? Kwa hali hii ya mambo, kumbe, ukweli wenyewe ni kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kuepuka kugusa au kutumia “alcohol” katika maisha yake ya kila siku.
Tunachotofautiana ni kiasi tu wala si suala la kuila na kunywa. Nielewe. Mnywaji wa pombe anaingiza nyingi tumboni mwake, na wewe unayekula mkate unaingiza tumboni pia. Hivi “alcohol” ya mkateni ya mwaka jana yote, na ya mwaka huu pia ingekuwa inasubiriana, ungekuwa umelewa chakari vile vile. Kumbe, unachodanganyika kwamba hulewi ni kwamba “alcohol” haisubiriani mwilini mwako. Bahati yako ndiyo hii tu. Kingine kinachokudanganya ni kwamba “alcohol” ya kwenye mkate haitiwi kwenye chupa au glasi ukaiona. Aidha, ni kwa sababu alcohol ya kwenye chupa inauzwa baa ambako huendi wakati “alcohol” ya kwenye mkate inauzwa dukani.
Kama unanifuatilia vyema, nadhani unaelewa kwa nini nasema katika dunia ya leo hakuna mjanja asiyegusana na pombe. Nakufundisha ufundishike, hivi narudia sababu. Ni kwa sababu mara nyingi mwanadamu hukutana na “alcohol” kwenye vyakula alavyo hata pengine pasipo yeye mwenyewe kujua.
Sikiliza tena. Mwanadamu anatumia “alcohol” kwenye mikate, kwenye sukari na kwenye vyakula vya nafaka na wanga pasipo kujua; anatumia “alcohol” kwenye vinywaji baridi mbalimbali pamoja na matunda pasipo kuhangaishwa kwa sababu kiasi cha “alcohol”(kwa Kiingereza “alcohol concentration”) ni kidogo tu, LAKINI KUWEPO IPO.
Na Waswahili
wanasema kama kitu kipo, kipo tu. La sivyo, mtu asiguse mkate, wala sukari,
vinywaji baridi na vyakula vya nafaka. Kwa nini? Kwa sababu katika vyote hivi,
“alcohol” ipo. Mtu anashambuliaje pombe ya kilabuni, wakati mwenyewe anaendelea
kula mikate, anatumia sukari katika chai, anakula mkate na anakula vyakula vya
nafaka.
Ni ujinga tu. Mwanadamu anapumbazika na kiasi cha “alcohol” kilichomo katika vitu alavyo kwa vile katika vyakula vingine huwapo kidogo kiasi cha yeye kutoonja vizuri uwepo wake. kumbe, ubishi juu ya “alcohol” unachochewa na ubishi wa kijinga tu.
Niache nikuongezee vitu. Kama umewahi kwenda hospitali ukapatiwa matibabu yenye kuhusisha ganzi, umeshagusana na kuitumia “alcohol”. Usishtuke, ndivyo ilivyo, ulikuwa ujingani tu. Zaidi ya hayo kama umewahi kutumia dawa hospitalini, hususan, zile zenye kukuletea usingizi, umeshagusana na “alcohol”. Usishtuke, ndivyo ilivyo, ulikuwa ujingani tu. Kumbe, ukitaka usigusane kabisa na “alcohol”, tangu sasa, usile mkate, usinywe vinywaji baridi, usitumie sukari, usile vyakula vya nafaka, usiende hospitalini na wala usipokee dawa za hospitalini.
Ndugu yangu, ukifaulu haya, utakuwa umejisogeza mahali fulani katika kuikwepa “alchohol”, la sivyo, funga domo lako. Ulikuwa ujingani tu. Lakini, ndiyo matokeo ya kukimbia masomo ya sayansi hayo. FUNGA DOMO LAKO MAANA HATUTAKI UTATANGAZIE KUTOKUJUA KWAKO SAYANSI. Nakusihi kwa heshima na taadhima, usilingane na mtu anayekataa kuitwa “baba” ila anataka sana aitwe “father”.
Mtu wa namna
hii ni kiroja cha karne ya ishirini na moja kwa sababu anachokikataa ni hicho
hicho anachokitumia. “Baba” na “father” maana ni ile ile. Kumbe, maskini hajui!
Lakini, basi, kwa ubishi wa aina hii tunawachefua watu, hasa wasomi wenye haki ya kututia Wakatoliki katika kapu la wajinga pia wakati si kweli.
Lakini, basi, kwa ubishi wa aina hii tunawachefua watu, hasa wasomi wenye haki ya kututia Wakatoliki katika kapu la wajinga pia wakati si kweli.
Wala
tusisahau, Kanisa Katoliki, tangu kale, lilikuwa likiongoza katika huduma ya
elimu katika shule za awali, chekechea, shule za msingi, sekondari, vyuo vya
ufundi na vyuo vikuu.
Leo, mimi nasikitika tunaporomoka kutoka katika tunu na huduma hii.
Leo, mimi nasikitika tunaporomoka kutoka katika tunu na huduma hii.
Kwa mfumo
wwa elimu usiompatia mtu elimu ya kujua mengi, wajinga wanaongezeka. Kwa bahati
mbaya, zamani wajinga walikuwa wazee, lakini siku hizi wajinga ni vijana. Hii
balaa kweli! Vijana ebu tumieni elimu yenu kugundua uongo mnaopatiwa. Elimu si
haramu. Nayo imetoka vile vile kwa Roho Mtakatifu.
Biblia inaweka sawa kabisa somo la kunywa na ulevi. Kunywa “alcohol” kwa wakati wake, kwa mfano kwenye sherehe, na kwa kiasi chake si haramu. Haramu ni kuhalifu wakati na kiasi hata kulewa. Ulevi ndiyo haramu. Na mtu kukitambua kiasi chake inategemea malezi na mtu mwenyewe anavyojikaza mbele ya kileo.
Wayahudi walipokuwa wanawafundisha vijana wao juu ya matumizi ya “alcohol” walikuwa wanasoma Zab 104:14-15 na kisha kusoma na kufafanua YbS 31:25-31. Zab 104:14-15 inasema: “Toka juu angani wainyeshea milima mvua, nayo dunia waitosheleza kwa baraka yako. Waotesha nyasi kwa ajili ya mifugo na mimea kwa matumizi ya binadamu ili naye ajipatie chakula chake ardhini; divai ya kumchangamsha, mafuta ya zeituni aya kumfurahisha na mkate wa kumpa nguvu”.
YbS 3:25-31 inasema: “Usijioneshe kwuwa hodari wa kunywa mvinyo, maana mvinyo umewaangamiza wengi. Tanuru hupima ugumu wa chuma na mvinyo hupima mioyo ya watu katika shindano la wenye kiburi. Mvinyo ni kama uhai kwa mtu ukinywa kwa kiasi. Maisha yafaa nini bila mvinyo? Imeumbwa iwafurahishe wanadamu. Kunywa mvinyo wakati wake na kwa kiasi, kwaleta shangwe moyoni na furaha rohoni. Lakini kunywa mvinyo kupita kiasi kunaleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha. Ulevi huongeza hasira ya mpuumbavu akajiumiza mwenyewe. Humdhoofisha na kumwongezea majeraha. Usimkaripie jirani yako kwenye mvinyo, wala usimdharau anapoifurahia karamu. Usimwambie neno la kumwonya wala umsimsumbue kwa kumtaka alipe deni”.
Kwisha kusoma YbS 31:25-31, marabi walikuwa wanatolea mfano kwa kuelezea pointi yao. Mfano wao ulikuwa huu:
“Mtu wa kwanza kupanda mzabibu alikuwa Nuhu. Nuhu alipokuwa anapanda mzabibu alikutwa na Shetani.
Shetani akamuuliza Nuhu, ‘Unafanya nini Nuhu?’
Nuhu akamjibu, ‘Ninapanda mzabibu.’
Shetani akamuuliza, ‘Mzabibu ni nini?’
Nuhu akamjibu, ‘Mzabibu ni mmea wa matunda, ukiwa mkubwa utazaa zabibu, hizo zabibu zikiiva, zitakamuliwa na kutoa mchuzi ambao tukiuchachusha utakuwa divai (mvinyo) ambayo Mungu amekusudia iwafurahishe wanadamu, wanaume na wanawake.’
Kusikia vile Shetani akasema, ‘Basi, mmea wako ni mmea mzuri. Niachie nikusaidie kidogo.’ Nuhu akamwachia mche Shetani kwa muda.
“Alichofanya Shetani katika mwanya huu ni kwenda porini kutafuta damu za wanyama aumwagilie mzabibu. Alienda akamchinja nyani, akaleta damu ya nyani akaja kuumwagilia mche. Akaenda mara ya pili, akamchinja simba, akaleta damu ya simba akaumwagilia mche.
Akarudi porini
mara ya tatu, akamchinja nguruwe na kuleta damu yake na kuumwagilia mche pia.
Kishapo, akamwachia Nuhu aendelee na matunzo ya mzabibu wake.
“Kweli, mzabibu ukakua na kutoa matunda, ndiyo zabibu. Nuhu akazikamua na kupata mchuzi wake. Akauchachusha mchuzi huo, ikawa divai nzuri, yaani yenye kilevi ndani yake (alcohol). Nuhu akawapa wanadamu divai aliyoitengeneza.
“Kweli, mzabibu ukakua na kutoa matunda, ndiyo zabibu. Nuhu akazikamua na kupata mchuzi wake. Akauchachusha mchuzi huo, ikawa divai nzuri, yaani yenye kilevi ndani yake (alcohol). Nuhu akawapa wanadamu divai aliyoitengeneza.
“Lakini, alipowapa watu wanywe divai yake, wanywaji wakaonesha tabia tatu tofauti kwa mwendo wa kupanda. Walipokunywa kiasi, wakaanza kuonesha tabia za nyani, kuchekacheka, kukaa juu ya meza, kujikunakuna na kadhalika.
“Walipozidisha hapo wakaanza tabia za ukali. Yakasikika maneno mengi sana, mathalani, ‘Nyamaza nitakupiga.’ ‘Nyamaza nitakuzibua, kwani hunijui mimi wewe! Mimi si mtu wa mchezo, nazaba pimbi kama wewe!’ na kadhalika. Walipoendelea tena kunywa, watu wakaanza kuonesha tabia za nguruwe. Baadhi wakawa wanatapika na wengine wakawa wanajikojolea nguoni mwao. Mwishowe, wengi wakalala chini na kugaagaa kwenye matapishi na haja zao”.
Kumbe, basi, kwa mfano huu, marabi waliwatanabaisha watu watambue kiasi gani cha divai ndiyo kiasi chao. Walisema KIASI ni kile kilichomfikisha mtu kwenye tabia za nyani tu, maana kuchekacheka, kukaa juu ya meza, kutembea tembea hapa na pale, kujikunakuna vyote havidhuru amani ya jamii. Lakini zaidi ya hapo, kunywa hata kufikia hatua ya simba ni vibaya kwani amani inawekwa rehani na mtu akirudi katika hali hiyo nyumbani kwake huweza kuwapiga watoto na mama yao. Hatimaye, hatua ya nguruwe ni fedheha tupu. Mtu akitapika, kujikojolea na kugaagaa kwenye matapishi yake huzuka kinyaa na kikwazo cha heshima kwa watoto, vijana, watu wazima na wazee.
Ndivyo hivi ilivyo, hata wewe mfano huu unaweza kukufaa. Naomba ukufae sana ili ujue kwamba uharamu wa ‘alcohol’ haipo katika uwapo wake bali katika kukosea wakati na kiasi. Kosa hili ni la mnywaji na siyo mtengenezaji. Ni kosa la mtumiaji na si kosa la kiwanda au mpishi. KIASI CHAKO ni kiasi kile kinachokufikisha kwenye tabia za nyani tu.
Zaidi ya
hapo usinywe. Tabia za simba haramu na hali kadhalika tabia za nguruwe.
Usivunje amani na hata kujiumiza mwenyewe na wala usijifedheheshe katika utu
wako. Usipokunywa kabisa heri, lakini kama utatumia uhuru na haki yako ya
kunywa, usipite kiasi cha nyani! Haya ndiyo mambo waliolewa Wayahudi wote na
ndiyo maana Yesu hakusita kutumia mwenyewe divai na wala hakusita kuwapa wale
waliokuwa kwenye harusi ya Kana (Yn 2:1-12) divai yenye kileo (oinos) na wala
hakuwapa juisi (gleukos). Asikudanganye mtu hapo.
Ndiyo kisa, kwa uelewa huu divai imepata sifa njema katika sehemu zifuatazo za Biblia takatifu: katika Agano la Kale: Mwa 14:18, 27:25.28.37, 49:11.12. Kut 29:40, Law 23;13, Hes 6:3.20, 15:5.7.10, 18:12.27, 28:7.14, Kum 7:13, 11:14, 12:17, 14:23.26, 18:4, 28:39.51. 29:6, 32:38, 33:28, Amu 9:13, 19:19, 1Sam 25:11.18, 2Sam 16:1.2, 2Fal 18:32, 1Nya 9:29, 27:27, 2Nya 2:10.15, 11:11, 31:5, 32:28, Ezra 6:9, 7:22, Neh 2:1, 5:11.18, 10:37.39, 13:5.12.15, Tob 1:7, 4:15.17, Ydt 10:5, 11:13, 12:1.13, 2 Mak 15:39, Ayu 1:13.18, Zab 4:7, 104:15, Mhu 2:3, 9:7, 10:19, Mit 3:10, 9:2.5, 31:6,Hek 2:7, Wim 1:2.4, 4:10, 5:1, 7:2.9, 8:2, YbS 9:10, 31:25-31, 32:6, 40:20, 40:20, Isa 5:12, 23:13, 25:6, 36:17, 55:1.12, 1 Sam 25:18, Jer 40:10.12, Dan 1:5.8.16, 10:3, Hos 2:22, 14:7, Joel 2:19.24, 3:18, Amo 6:6, 9:14, Mic 2:11, 6:13, Zep 1:13, Hag 1:11, 2:12 na Zec 9:17, 10:7
Katika Agano Jipya: Mt 9:17, 27:34.48, Mk 2:22, 15:23.36, Lk 5:37-339, 7:33, 10:34, Yn 2:3.9-10, 4:46, 19:29-30 na 1Tim 5:23.
Je, umechoka kwa orodha ndefu? Naona leo nimekusheheneza kwa nukuu, je upo nami bado? Lakini nakuomba usichoke maana namalizia mada yangu sasa!
Ndugu yangu, ukichambua sehemu hizi utaona kwamba divai au mvinyo imetajwa kuwa na manufaa kwa vipengele sita. Mosi, ni sehemu ya lishe ya binadamu (Mwa 27:25.28, 27:37). Pili, ni kitu cha kuwafurahisha wanadamu wake kwa waume (Zab 104:15, Yn 2:3.9-10). Tatu, ni dawa (Lk 10:34, 1Tim 5:23). Nne, ni kitu cha kuwapa nguvu waliochoka 2Sam 16:2. Tano, ni kitu cha kutulizia maumivu (Mt 27:34.48 Yn 19:29-30).
Sita, ina
matumizi ya kisadaka (Mwa 14:18). Nahitimisha kwa suala lile la ubishi wa
kijinga. Nimeshazungumzia kwa urefu ushahidi wa kwanza wa ujinga. Nimeonesha
kwamba ushahidi wa kwanza ni ule wa mtu kutokujua kwamba hajaweza kuikwepa
“alcohol” (mvinyo, divai au pombe) maishani mwake kwani ipo kwenye vitu vingi
anavyovitumia lakini kwa kuwa hajui anadhani hajaila wala kuigusa.
Kwa kukutajia vipengele sita vya manufaa ya divai, kama vinavyochambulika katika nukuu nyingi za Biblia, nimekuletea ushahidi wa pili wa ubishi wa kijinga. Ni hivi, mtu anapobishia matumizi ya mvinyo kama mvinyo bila kuisoma Biblia vizuri anaonesha ujinga wake kwa namna ya pili.
Inakuwaje
mtu anayejitambua arukie kwenye ulevi tu huku akifunika vipengele vyote vya
manufaa kana kwamba amelewa? Inakuwaje mtu anaangalia matumizi mabaya tu?
Inakuwaje mtu anaangalia hasara zaidi kuliko manufaa? Inakuwaje mtu anaangalia
hasi zaidi kuliko chanya iliyo kubwa zaidi?
Kumbe, hapo ndipo tunapopata ushahidi wa aina ya pili wa ubishi wa kijinga. Kupigania kukataza pombe ni kosa katika fikra.
Kumbe, hapo ndipo tunapopata ushahidi wa aina ya pili wa ubishi wa kijinga. Kupigania kukataza pombe ni kosa katika fikra.
Manufaa ya
“alcohol” si kulewa tu. Matumizi ya “alcohol” si ulevi. Yaani ni kama mtu
angalipogombea tupige marufuku uwapo wa bodaboda, magari na ndege kwa sababu
zikitokea ajali vyombo hivyo vinaua watu wengi, huku akisahau kwamba vyombo
hivyo vikiendeshwa vyema vinaturahisishia wanadamu usafiri, vinatubebea mizigo
yetu mizito, inatuwahishia wagonjwa wetu kwenye matibabu, vinatulea furaha
katika usafiri na kadhalika. Matumizi ya vyombo vya usafiri si ajali, kama
ilivyo matumizi ya vyakula si ulafi. Kumbe tupunguze ubishi wa kijinga.
Tutenganishe matumizi mazuri na matumizi mabaya kusudi tutende haki. Lawama si
kwa kitu ila kwa mwanadamu anayekitumia.
Hata kisu
kinaweza kukata matunda au nyama ipikwe lakini kinaweza kutumiwa kujeruhi na
kuchinja wanadamu. Lakini katika mkabala huu, hatuwezi kupiga marufuku uwapo wa
visu duniani. Mkanda wa suruali unabana suruali ili isimvuke mtu hadharani,
lakini unaweza kutumika katika kujinyonga hadi kufa. Hata hivyo, katika mkabala
huu hatuwezi kupiga marufuku mikanda duniani. Nadhani mnipata uzuri! Kama
ndivyo, nawasihini tuache ubishi wa kijinga.
Kwa mara nyingine kwa herini kwa muda! Pd. Titus Amigu.
Kwa mara nyingine kwa herini kwa muda! Pd. Titus Amigu.
Post a Comment