Chama
cha Soka cha Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini (sorufa); leo hii
kimegawa Mipira 10 kwa timu Tano za watoto wadogo.
Timu
zilizonufaika na mipira hiyo toka TFF ni Namiholo Queens (Peramiho), Jenista
Kids (Nakauga), Toto Fc, Young Kids ya Mharule pamoja na Red Kids ya Peramiho
ambapo kila timu imepata mipira miwili.
Mgeni
Rasmi katika zoezi hilo ni Mwenyekiti wa serikali wa Peramiho A Mh. David
Kapinda. Mipira hiyo ni ile 100 iliyotolewa na TFF kila mkoa kwa ajili ya
kuendeleza soka la vijana.
Post a Comment