Ads (728x90)

Powered by Blogger.


                                             Utangulizi
Hapo mwanzo  kabila la  Wazulu (Ama-Zulu) lilikuwa ni kabila dogo sana. Kiidadi lilikuwa na wakazi wapatao 2000.

Kabila hilo lilikuja kupata umaarufu chini ya utawala wa Mfalme Tshaka. Tshaka Bin Senzangakona Mwanga wa Umnyama bin Ndaba bin Mpunga bin Mageba bin Zulu Malandela.

Inaelezwa kwamba Malandela aliishi kipindi cha pili cha karne  ya 16 kama ilivyoonyeshwa katika orodha ya ukoo wake hapo juu, katika orodha hiyo inaonyesha wazi kabisa kwamba Zulu alikuwa ni babu ya Tshaka na kabila lote lilipata jina kutoka kwa huyo hata baada ya yeye.
 

Jina Zulu lilikuwa  ni jina alilopewe mtumishi mpendwa wa Tshaka. Mtumishi huyo alipata jina hilo kutoka kwa Tshaka mwenyewe mara baada ya kuonyesha uodari mkubwa vitani katika kutetea  Ufalme wa Shaka.
Mababu wa Tshaka waliishi Kusini mwa White Umfolozi karibu na mito Mkumbane pamoja Uzololo na walizikwa pale mahali palipoitwa Makosini. Tshaka alipata mafunzo ya kijeshi kutoka katika kikosi cha jeshi la Dingiswayo ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi.

Dingiswayo alikuwa pia mshauri wa Tshaka katika masuala yahusuyo ushujaa na mbinu za kijeshi.

Msaada wa kijeshi aliopata Mundisho toka kwa Tshaka
Baada ya kuuawa Dingiswayo mrithi wake na kaka yake Mundisho alikuwa bado ukimbizini akiishi na Wazulu huko Zululand, Tshaka alifaulu kutoa msaada wa kijeshi ili kumfadhili Mundisho.

Basi Tshaka akafanya vita dhidi ya Zwide. Tshaka alitambua wazi kwamba jeshi la Zwide lilikuwa imara kuliko jeshi lake.
Hapo alilazimika kutumia maarifa pia kufanya jitihada ili aweze kulishinda jeshi la Zwide.

Mwanzoni mwa vita Tshaka alilizuia jeshi la Zwide lilipotaka kupigana naye, lakini alilielekeza jeshi lake upande wa kusini na kuuvuka mto Tugela kwa vile jeshi la Zwide  lilikuwa  hodari na lenye nguvu kuliko la Tshaka.

Katika kufanya hivi Tshaka aliweza kuliongoza jeshi lake ili kuharibu mazao yaliyokuwa mashambani katika njia iliyokisiwa kwamba kikosi cha askari wa Zwide kilipanga kupita.

Askari  wa Tshaka walichoma  moto mashamba  na kuharibu mazao ambayo yalikuwa ni tegemeo kubwa kwa jeshi la Zwide ambalo halikubeba chakula cha kutosha katika vita ile.
Wao walitegemea kupora mazao ambayo waliyaona njiani ili kuendelea na mapigano katika vita.

Kwa muda fulani jeshi la Zwide lilifaulu kumudu vita lakini kwa vile hawakuwa na chakula cha kutosha  na njiani jeshi la Tshaka lilishasambaratisha mazao yote, hali hiyo ilipelekea jeshi la Zwide kupata shida kisha likarudi nyuma.
Jeshi la Zwide lilifika eneo la mto Umhlaluzi huku likiwa katika hatari ya kushinda na njaa, Tshaka akapata nafasi ya kulivamia jeshi hilo na akaliteketeza.

Zwide akiwa na wanajeshi baadhi ambao walivumilia njaa na kuendelea kuishi walikimbilia katika nchi ya Wathonga na alipofika huko kifo kimpata. Tshaka sasa alikuwa mtawala wa Zululand yote.

Vita kati ya waana wa Zwide

Baada ya kifo cha Zwide watoto wake Sikunyama (Sikunyane) na Somabunga  walianzisha vita ya wao kwa wao ili kugombania urithi wa ufalme. Katika vita hiyo aliyeshindwa ni Somambunga na mshindi alikuwa ni kaka yake aliyeitwa Sikunyama.

Hapo Somabunga alitoroka kuelekea kwa Tshaka ambaye alimruhusu kuishi katika nchi yake lakini nchi ya Wandwandwe kama mwakilishi wake.

Sikumanya kama Mfalme wa Wandwandwe  ambaye alikimbilia katika nchi ya Thongaland alitaka kuirudisha nchi yake kwa nguvu iliyotekwa zamani.

Aliingia Zululand kupitia sehemu iliyokaliwa na watu wengi akiwa na jeshi kubwa sana. Baadhi ya viongozi wa vita aliokuwa nao ni pamoja na Zwangendaba bn Hlachwayo ambaye pia alipigana upande wa Zwide kwenye mto Mhlatuzi na baadaye alikuwa pia kiongozi wa Wangoni huko Afrika ya kati.

Ngaba bn Mbekane Soshangane mdogo wake Zwide na Sobuza bin Ndungunye ambaye alikuwa Mfalme wa Swaziland.

Vita hii dhidi ya Tshaka iliyofanywa mwaka 1824 iliyoisha kwa kushindwa kabisa kwa Sikunyama ambaye aliuawa kwenye vita akiwa kikosini baadhi ya askari zake walirudi katika nchi yao ya Thongaland. Tshaka alikuwa na ndugu aliowaita kaka zake, nao walikuwa watatu majina yao ni Dingana, Umhlanga na Umpande, kwa vile Tshaka alizidi kuwa katili mara kwa mara  kwa watu wake alichukiwa huku wakimponda juu ya utawala wake.

Mwishowe aliuawa na  ndugu zake kaka zake akina Dingana na Umhlangana. mambo hayo yalitokea mwaka 1828.

Baadhi ya wafalme waliotawala nchi ya  Zululand

Baada ya Tshaka: Dingana Kaka ya Tshaka baada ya kumuua kaka yake alikuwa pia mpinzani wake Umhlanga pia alikuwa mtu aliyeupata ufalme kwa kung’ang’ania katika nchi ya Wazulu.
Alikimbilia Swaziland na kutoroka ujio wa Boers wenyeji wa kidachi wakaaji wa Afrika ya Kusini na hivyo kuuawa kule mwaka 1840.

Baadaye alirithi mtu aliyeitwa Upande ambaye alikuwa mdogo wa Dingana aliyekufa mwaka 1872.

Huyo upande alikuwa na waana wawili nao ni Cetshwaya na Umbulazi ambaye naye aliuawa wakati wa vita ya kutafuta ushindi wa kupigania nchi: Cetshwaya naye alikufa mwaka 1884 na akazikwa karibu na Nkandhla kwenye bonde la mto Insuzi.

Dinizulu mwana wa Cetshwayo alirithiwa na Solomon mwana wa Dinizulu na alikuwa Mfalme mpaka mwaka 1913.

Habari za wazulu, Wngoni wa Tanganyika na Wamatebele.......

(a)Wazulu na Wangoni wa Tanganyika

Jina zulu linasikika nchi nzima ya Tanganyika . Zulu Gama alikuwa ni chifu ambaye aliwaongoza Wangoni kutoka Afrika ya kati hadi Afrika ya Mshariki  akiwa na mtu wa karibu sana rafiki na shemeji yake mtu aliyeitwa Mbonane Tawete.

Zululand waliishi watu walioitwa U-Fulatela na U-Baleni (CF. Callaway, Religions System of Amazulu Uk. 13 na 102).

Majina hayo yanatumika kwenye koo za akina Gama hapa Tanganyika. Sitole na Isilangani yalikuwa ni majina ya ukoo wa Watale huko Zululand na akina Mlangeni.

Kufanana kwa majina haya kunaleta muunganiko wa kihistoria kati ya Wangoni wa huku Tanganyika na wenyeji wa Zululand.

(b)Wamatebele

Wamatebele (Ama-Ndebele-Abakwa-Zulu) sasa hivi ni mojawapo ya makabila makubwa katika Rhodesia ya kusini kwa sasa (Zimbabwe) hao walikuwa wahamiaji kutoka nchi ya Zululand.

Wakati bado wapo katika nchi ya Zululand watu hao waliishi Kaskazini kwenye miteremko ya milima ya Ingome. Chifu wao aliyeitwa Msilikazi Kumalo mwana wa Matshobana, alikuwa mjukuu wa  Zwide na Mama yake aliitwa Nompetu.

Zwide aliposhindwa katika jeshi au vita kwenye mto Umhlatuzi, Msilikazi mara moja alijisalimisha kwa Tshaka, kwa vile kabila lake lilikuwa dogo likawekwa chini ya ulinzi wa jeshi la Wazulu.
Baadhi ya watu wake waliongezwa kwenye kikosi cha jeshi la Wazulu ambalo lilikuwa na makao yake makuu huko Bulawayo (Zululand) kwenye wilaya kati ya mto Umhlatusi na Umlalazi.

Baada ya muda fulani Msilikazi hakuaminika kwa Tshaka na kupata fedheha kutokana na masuala ya kivita, kwa kuhofia usalama wake ilimlazimu kuachia nchi ya Zululand akiwa na watu wapatao 15000 na akasafiri umbali mrefu kuelekea Drankensberg ndani ya nchi ya Transvaal.

Kila mara jeshi lake lilipopita lilifanya mauaji ya kinyama na kuharibu kabisa makazi ya watu. Huko Kaskazini Magharibi ya Transvaal Msilikazi aliweka kituo cha jeshi mahali palipoitwa Mosenga.

Kwa kuwa alikuwa tishio akaja kufanya uhasama na wale Boers na kulazimika kuihama Transvaal kisha yeye na jeshi lake wakavamia Rhodesia na kukaa sehemu ya kusini mahali ambapo wenyeji toka Zululand wanaiishi mpaka leo.

Msilikazi alijenga mji mkuu na kuweka makao ya jeshi na kupaita “Bulawayo”. katika makao yao mapya mara nyingi waliwashambulia majirani na kuleta maafa kwa wenyeji kila mahali.
Msilikazi alikufa mwaka 1870 na alirithiwa na mwana wake aliyeitwa Lubengula. Baada ya kifo cha Lubengula mwaka 1893 kabila hilo lilipoteza uhuru wake na nchi ikatawaliwa na Waingereza.


Post a Comment