Ads (728x90)

Powered by Blogger.




 
Alizaliwa katika mji wa Florensi, Aprili 2 mwaka 1566. Baba yake yake aliitwa Kamilli di Gerride Pazzi na mama yake aliitwa Magdalena walikuwa watu wenye uwezo kiuchumi.
Alibatizwa mapema siku iliyofuata ya tarehe 3 Aprili katika kanisa la Mtk.Yohane Mbatizaji, alianza kuonyesha mapendo ya sakramenti takatifu tangu alipokuwa mdogo, alipokea komunyo takatifu akiwa na miaka 10 na aliamua kuweka nadhiri ya milele ya ubikira kwa Mungu.

Alipata kwa mara ya kwanza hali ya juu ya muungano wa kiroho (ecstasy) siku ya sikukuu ya Mtakatifu Andrea mtume mbele ya mama yake alipokuwa katika bustani.
Tarehe 14 mwaka 1582 aliingia katika Monasteri ya wakarmeli ya mtakatifu maria wa malaika akiwa na miaka 17 kwa siku 15 ili kuona kama anaweza kuendana na sheria zao na kutaka kujua kwamba hana wito toka kwa Mungu.
Sheria za utawani zilimkidhi haja yake yake ya kuwa mtawa na hivyo aliamua kuchagua maisha hayo ya utawa katika monasteri. Alipewa vazi la shirika Januari, 1583 na kuchagua jina la sista maria Magdalena na kuanza mwaka wa unovisi.
Mungu alimjalia neema kwa kumtokea mara nyingi na pia kumtolea siri za moyo wake.
Mnamo mwaka 1584 alipata ugonjwa wa hatari, alikuwa na homa kali pamoja na kukohoa sana, alikuwa na maumivu makali sehemu ya kifua chake na chini ya mbavu zake.
Usiku na mchana alibaki amekaa kwenye kitanda bila kulala kwa sababu ya kukohoa. Na mara chache sana alipata usingizi. Alikuwa mgonjwa kwa miezi miwili, mkuu wake na mlezi wake waliamua kumruhusu afunge nadhiri kwa sababu ya hali yake ilizidi kuwa mbaya na alikuwa kama mgonjwa anayekaribia kufa.
Iilikuwa sikukuu ya utatu mtakatifu tarehe 27 mei 1584. Baada ya nadhiri zake alirudishwa kwenye chumba chake cha wagonjwa na kuanzia hapo alianza kipindi cha kushangaza cha kupata hali ya juu ya muungano wa kiroho na kupata maono mbalimbali.
Kila siku baada ya komunyo alibaki katika hali hiyo ya muunganiko kiroho (hali ya kuwa katika ulimwengu wa kiroho) aliweza kukaa kwa masaa mawili mpaka matatu.
Na hali hii ilimchukua kwa siku arobaini. Aliweza kupata maono ya mateso ya bwana, kubadilishana moyo wake na ule wa yesu, kupata madonda matakatifu.
Aliponywa mnamo Julai 16 na maombezi ya Bikra maria.
Kuanzia hapo maisha yake yalikuwa na mfululizo wa maono na muunganiko kiroho.
Tarehe 17 Mei 1585 aliweza kuwa na muda mrefu toka hali ya kawaida hadi kufikia hali ya juu ya muungano kiroho na hali hiyo ilianza Ijumaa mchana na iliendela kwa muda wa masaa arobaini mpaka siku ya Jumapili asubuhi.
Alipokea amri toka kwa bwana kuchukua mkate na maji kama chakula chake isipokuwa siku ya Jumapili na siku takatifu.
Pia alikuwa na uwezo wa kutabiri mambo yajayo na kusoma siri za moyoni. Aliweza kupata mzunguko mkubwa wa kuunganika kiroho bila kiusimama kwa muda wa siku nane isipokuwa masaa mawili tu kila siku ambayo yalikuwa kwa ajili ya kusali, kupata chakula na kupumzika kidogo.

Mara saba aliweza kumpokea roho mtakatifu kwa hali tofauti hasa asubuhi. Mungu alimfunulia kwamba kanisa linahitaji marekebisho na wote wanahitajika katika kushirikiana naye katika hilo, na alikuwa na utume maalumu kuwakumbusha watawa na watu wa hadhi ya juu wa kanisa majukumu yao. Alifadhaika kwa hali hiyo kwa sababu ingeweza kumwathiri na unyenyekevu, aliongea na mapadre wake wa kiroho na wote walimshauri kufuata amri ya Mungu bila kusita, alisali na kuliombea kanisa lipate kurekebishwa.
Muda mwingi alikuwa yupo katika hali ya kimungu na maono, mara kwa mara alionekana akipiga magoti kwenye kitanda chake na kuwa katika hali ya juu ya kiroho.
Alipata neema nyingi toka kwa mungu hasa kwa vitu vya kiroho, muda mwingine wakati alipokouwa amelala usingizi hali hiyo ya muunganiko kiroho ilimjia, hasa wakati wa usiku na kuanza kuongea vitu vya kimungu kwa sauti kubwa hadi wenzake wanovisi waliokuwa wamelala naye kwenye chumba waliamka na kumzunguka na kusikiliza mambo mazuri aliyokuwa anaongea ya kimungu. Alifariki mwaka 1607. Alizikwa na baada ya miaka miwili, mwili wake ulianza kutoa harufu nzuri ya manukato, alitangazwa mtakatifu mwaka 1669.
Imetayarishwa na frateri Theophil. C. Wabukundi, OCD. Wa shirika la karmeli, Kola- Morogoro, theoocd@gamil.com, 0764038597, Kwa msaada wa vitabu vya, Oxford Dictionary of saints na David farmer, saints Companion for Each day na A.J.M. Mausolfe na J.K. Mausolfe, na


Post a Comment