Ads (728x90)

Powered by Blogger.


Timu ya Afya Sports Club ilianzishwa kati ya mwaka 1986-1988 ikiwahusisha zaidi Wafanyakazi wa Hospitali ya Mtakatifu Josefu-Peramiho. 


Ambapo mwaka 1989-1990 Afya SC ilishiriki Mashindano ya Ligi Daraja la Nne kwa mara ya Kwanza.

Mnamo mwaka 1991-1992 ilishiriki tena Mashindano ya Ligi Daraja la Nne na ilipanda hadi hatua ya Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Wilaya.
Mwaka 1993-1994 Afya SC ilifanikiwa kushiriki Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Mkoa iliyofanyika katika Wilaya ya Tunduru.

Mwaka 1995-1996 ilifanikiwa kushiriki Fainali Mashidano ya Ligi Daraja la Tatu Ngazi ya Taifa Kanda ya Kusini ambayo yalifanyika Wilayani Nachingwea.

Mwaka 1997-1998 Afya SC ilifanikiwa kucheza Ligi Daraja la Pili Ngazi ya Kanda ya Kusini Mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Majimaji Mkoani Ruvuma.

Mwaka 1999-2000 Timu ya Afya SC ilishiriki Mashindano ya Ligi Daraja la Pili katika hatua ya Fainali Kitaifa ambayo yalifanyika Mkoani Mtwara katika Uwanja wa Umoja.

Baada ya kutoka katika Ligi hiyo, Wazo la kuanzisha Mashindano ya Ansgar Cup Tarafa ya Ruvuma lilitolewa na Dk. Ansgar Stuffe OSB ambaye ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Mtakatifu Josefu-Peramiho, kati ya mwaka 2000 – 2002.
 
Mashindano ambayo yalilenga kuhusisha Michezo mbalimbali ikiwepo Mchezo wa Soka (Football) na Mchezo wa Pete (Netball).

Hivyo Mkurugezi aliitisha kikao cha Madiwani na Viongozi wa Timu ya Afya kujadili uwezekano wa kuwa na Ligi Ngazi ya Tarafa ya Ruvuma na yeye kuwa Mfadhili na pia katika Kikao hicho alihamasisha kuwepo na uwanja wa kufanyia Mashindano hayo.

Yafuatayo ni malengo yaliyopendekezwa na Mkurugenzi wa Mashindano haya makubwa ndani ya Mkoa wa Ruvuma:
·        Kuleta burudani
·        Kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji
·        Kupunguza vitendo hatarishi, hasa kuzuia maambukizi ya gonjwa hatari la UKIMWI.
·        Kutoa fursa ya kufanyika biashara ndogondogo ili kujikimu kiuchumi na
·        Kudumisha mahusiano baina ya Jamii za ndani ya Tarafa ya Ruvuma.

Wazo hilo lilipokelewa kwa mikono miwili na wajumbe wote waliohudhuria katika kikao hicho kilichofanyika kwa mara ya kwanza hapa Peramiho. 

Jina la Mashindano Ansgar Cup na jina la Uwanja Ansgar Stadium lilitolewa na wajumbe waliohudhuria kwenye kikao hicho cha kwanza ambao ni Madiwani, Watendaji, Maafisa Elimu Kata na Uongozi wa timu ya Hospitali ya Peramiho (Afya SC).

VIONGOZI WA MWANZO WA ANSGAR CUP (UPANDE WA UFADHILI)
Mwenyekiti – Mr. Emeran Ndunguru
Makamu Mwenyekiti – Dk. Magnus Mwanyika
Katibu – Mr. Atilio nzota
Katibu Msaidizi – Mr. Christandus Kinyero
Katibu Mwenezi- Mr. Columban Lugendo
Mweka Hazina (Mhasibu)- Mr. Romanus Mgimba


VIONGOZI WA SASA (UPANDE WA UFADHILI)
Mwenyekiti – Mr. Thadei Mgaya
Makamu Mwenyekiti – Dk. Magnus Mwanyika
Katibu – Mr. Atilio Nzota
Katibu Msaidizi – Mr. Christandus Kinyero
Katibu Mwenezi – Mr. Dickson Komba
Mweka Hazina (Mhasibu)-Mr.Romanus Mgimba
Mratibu-Mr. Emeran Ndunguru
 
Kwa kipindi cha miaka 16, toka mwaka 2002 hadi hivi sasa Ansgar Cup Tarafa ya Ruvuma, imekuwa ikifanyika kwa mafanikio makubwa mfululizo. 

Kwa takriban miaka 16 iliyopita Ansgar Cup imekuwa ikiendelea katika Tarafa ya Ruvuma ambapo Washindi wa kwanza wamekuwa wakizawadiwa Fedha na Kikombe huku Makamu bingwa na Mshindi wa tatu wakizawadiwa Fedha taslimu.

Zawadi zote za Washindi zimekuwa zikiwiana katika Michezo yote miwili yaani Football na Netball.

Ikumbukwe kuwa Mkurugenzi wa Mashindano haya amekuwa akifadhili Mashindano haya tangu hatua za Ngazi ya Kata ambapo amekuwa akitoa Vifaa vya Michezo kwa Timu shiriki na zawadi nyinginezo kwa Washindi katika kila Kata.


MSIMAMO WA WASHINDI TANGU MWAKA 2012-2017
MWAKA
TIMU
KATA
2012
PERAMIHO STARS
MAPOSENI
2013
LITISHA
LITISHA
2014
LIKUYU FC
LILAMBO
2015
MGAZINI FC
KILAGANO
2016
   KILAGANO FC
       KILAGANO
2017
     CHABRUMA FC
       LILAMBO

RATIBA YA ANSGAR CUP TARAFA YA RUVUMA 2018

APRILI 15, 2018: LITISHA ‘A’ VS MAPOSENI   (14:00 PM)
                                     PERAMIHO VS M/NGINDO (16:00 PM)
APRILI 21, 2018:  LITISHA ‘B’ VS LIGANGA      (14:00 PM)
                                     PARANGU VS KILAGANO     (16:00 PM)
APRILI 22, 2018:  PERAMIHO VS LITISHA ‘A’  (14:00 PM)
                                     M/NGINDO VS MAPOSENI  (16:00 PM)
APRILI 28, 2018:  PARANGU VS LIGANGA        (14:00 PM)
                                     LITISHA ‘B’ VS KILAGANO  (16:00 PM)
APRILI 29, 2018:  LITISHA ‘A” VS M/NGINDO (14:00 PM)
                                     MAPOSENI VS PERAMIHO  (16:00 PM)
MEI  06, 2018:       PARANGU VS LITISHA ‘B’    (14:00 PM)
                                     KILAGANO VS LIGANGA      (14:00 PM)

NUSU FAINALI

MEI  13, 2018:     MSHINDI WA KWANZA KUNDA  A
                                                                 VS  
                                  MSHINDI WA PILI KUNDI B (14:00 PM) 

                                  MSHINDI WA KWANZA KUNDI B
                                                                 VS 
                                  MSHINDI WA PILI KUNDI A (16:00 PM)

MSHINDI WA TATU
MEI  19, 2018:  ZITAKAZOPEPETWA NUSU FAINALI
MECHI YA FAINALI
MSHINDI WA NUSU FAINALI YA KWANZA VS MSHINDI WA NUSU FAINALI YA PILI
ITAPIGWA MEI 20, 2018 (SIKU YA JUMAPILI) SAA 16:00 PM.

Kwa mwaka huu (Mwaka 2018) Uongozi wa Ansgar Cup Tarafa ya Ruvuma umeyaboresha Mashindano haya kwa kurusha Matangazo ya moja kwa moja ya Redio lakini pia kuripoti Magazeti na kwenye Mitandao ya Kijamii hasa Peramiho Publications (Facebook) na Blog www.peramihopublications@blogspot.com. 

Ambapo katika Mchezo wa Ufunguzi kati ya Timu mwenyeji (Peramiho) dhidi ya Kata ya Mpandangindo mchezo utatangazwa moja kwa moja na Kituo cha Redio cha Jogoo FM na fainali itarushwa na Key FM zote za Mkoa wa Ruvuma.

Pia Uongozi Mpya wa Mashindano umejipanga kuandaa Kalenda za Matukio ya Ligi ambapo kutakuwepo na Wapiga Picha katika kila Mchezo watakaopiga Picha Matukio yote ya Ligi na kujumuishwa katika Kalenda hizo hapo mwakani 2019. 

MICHEZO NI AFYA, ANSGAR CUP IDUMISHWE
Imeandaliwa na Mr. Thadei W. Mgaya
Mwenyekiti wa mpya wa ANSGAR CUP .

 





Post a Comment